Haya yanakuja huku utawala katili wa Israel ukizidisha mashambulizi ya kinyama na kuua raia wasio na hatia huko Gaza na Lebanon, na vita vikiendelea kati ya Russia na Ukraine.
Trump amesema: "Mashariki ya Kati inalipuka, na tunaweza kuwa kwenye ncha ya kutumbukia kwenye Vita vya Tatu vya Dunia; Ikulu ya White House haijui la kufanya."
Kura ya maoni iliyofanywa na CNN kwa ushirikiano na SSRS - iliyochapishwa leo, Jumanne - inaonyesha kuwa Trump na mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris, wanakabana koo katika uchunguzi wa maoni ya wapiga kura watarajiwa kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Novemba 5 mwaka huu.
CNN imeripoti kuwa, kura hiyo iliyofanywa kuanzia Septemba 19 hadi 22, inaonyesha kuwa Harris amepata 48% na Trump 47%, wiki 6 kabla ya mwisho wa kampeni za uchaguzi wa rais.
Majuzi, gazeti la The New York Times liliripoti kwamba kuna wapiga kura ambao hawajaamua ni nani watampigia kura katika uchaguzi wa urais wa Marekani, na wengi wao ni vijana, Wamarekani weusi, na Wahispania, na wanaweza kubadili mwelekeo wa matokeo ya uchaguzi huo.
342/